Fahamu hatua rahisi jinsi ya kutangaza Biashara Yako Kupitia mtandao wa Zoom Tanzania
Mfanyabiashara yeyote analengo la kuhakikisha biashara yake inawafikia wateja wengi iwezekanavyo ili aweze kuuza bidhaa zake kwa njia rahisi na salama iwezekanavyo. Kama mfanyabiashara au mjasiriamali, ni muhimu kuhakikisha kuwa biashara yako inakwenda na nyakati. Katika nyakati hizi za teknolojia, idadi kubwa ya wateja wa biashara mbalimbali ni watumiaji wakubwa wa mtandao. Ndio maana, katika nyakati hizi ni muhimu kuwafuata wateja walipo, kwenye mitandao. Mfano mzuri ni Mtandao wa Zoom Tanzania unaowakutanisha wauzaji na wanunuzi toka mwaka 2009. Katika mtandao huu, wanunuzi huenda kwa leongo moja la kufanya manunuzi na wauzaji kutangaza bidhaa zake.
Fikiria pale ambapo mtu ana shida ya kununua gari ambalo wewe unauza. Anaingia mtandaoni, anaandika jina la gari, mfano Rav 4. Anakuta umeweka picha, maelezo ya gari na bei, analipenda kisha anachukua namba yako na anakupigia halafu mnakamilisha biashara.. Ni rahisi hivyo.
Hatua za Kutangaza katika Mtandao wa ZoomTanzania
Hatua ya kwanza kabisa ya kutangaza bidhaa yako ni kuwa na akaunti Zoom Tanzania. Ikiwa unataka kuanza kufungua akaunti, unaweza ukatumia ukurasa huu. Maelezo yanayohitajika ni majina yako na namba yako ya simu kwa ajili ya kuthibitisha uhalali wako na wa akaunti yako. Pia unaweza ukatumia akaunti yako ya Facebook kujisajili.
Mtandao ni kama soko kubwa sana ambalo kuna kila kitu ndani yake. Kama bidhaa zisipowekwa kwa mpangilio, basi itakuwa vigumu kwa mteja kuziona bidhaa anazozitaka. Ndio maana, hatua inayofuata baada ya kuwa na akaunti, ni kuchagua bidhaa unayotaka kuuza. Hakikisha unachagua kipengele husika cha bidhaa unayotaka kuuza. Ni muhimu kufanya hivi ili kurahisisha uuzaji wa bidhaa yako. We fikiria, mteja anatafuta viatu halafu wewe umeviweka sehemu ya magari. Atavipata kweli?
Baada ya kuchagua kundi la bidhaa unayouza, basi ni vyema kuielezea bidhaa yako ili maelezo yako yamsaidia mteja anayeichagua. Fikiria maswali wanayouliza wakija kununua dukani? Mbona hii bidhaa kubwa sana, mbona rangi imepauka, hii ina uzito gani, imetumika muda gani n.k. Haya majibu yanahitajika kuwa katika maelezo.
Mara zote unapouza bidhaa mtandaoni kumbuka mteja anakuwa hana namna yeyote ya kujua ubora wa bidhaa unayouza. Tofauti na maduka ya kawaida ambapo anaweza akaona kitu, akashika na kuamua kununua au kutokununua, mteja hawezi kupata uwezo wa kuangalia bidhaa kama dukani. Picha tu ndio zitamfanya mteja aamue kununua bidhaa yako. Hivyo ni muhimu sana kama picha utakayoitumia nzuri na inayojitosheleza. We fikiria, unapita mtandaoni ukakuta mtu anauza gari lakini ameweka picha mbaya, iko moja na haionekani vizuri, utanunua? Hivyo hivyo ndio wateja wako watakavyokwepa tangazo lako ikiwa hujaweka picha nzuri. Tafuta mazingira mazuri ya kupigia picha yenye mwanga, nafasi na mwonekano mzuri.
Baada ya kufungua akauti, na kuweka tangazo lako, kinachobakia sasa ni wa timu za Zoom Tanzania kuhakiki tangazo lako. Hii hufanyika ili kupunguza uwezekano wa kuwepo kwa matangazo ya matapeli katika mtandao wa Zoom Tanzania. Timu ya kuhakiki matangazo itakagua endapo tangazo lako lina makosa madogo yanayoweza kuwachanganya wanunuaji. Baada ya muda mchache kama wa masaa mawili, tangazo lako litathibitishwa.
Baada ya hapo sasa kazi ni kwako. Subiri wateja kutoka sehemu mbalimbali waanze kutiririki. Kumbuka, unahitaki kuwa na hudumu nzuri kwa wateja wako. Mfano, kama wamepiga simu kutoka eneo ambalo si mbali sana na duka lako, unaweza ukaamua kuwafanyia ofa ya kufikisha bidhaa mpaka walipo bure kabisa. Au unaweza ukawapa ofa ya nyongeza, tuseme cover la simu la bure kama wakinunua simu toka kwako. Unadhani hawatarudi tena? Usiache fursa hii. Huu ndio wakati wako na biashara yako! Ingia Zoom Tanzania sasa uanze kutangaza biashara yako.
Comments