Kisonono au kisalisali ni ugonjwa wa zinaa ambao usababishwa na bacteria wanaofahamika kisayansi Kama Neisseria gonorrhoea.kisononi mara nyingi huambukiza urethra(mirija Kati ya kibofu cha mkojo na ngozi) pamoja na shingo ya kizazi kwa wanawake.Dalili za kawaida ni Maumivu wakati kukojoa na uchafu kutoka kwenye mrija wa mkojo.watu wengi wenye kisonono hawana dalili,na hugunduliwa kuwa na hali hii kwa vipimo vya uchunguzi