Tatizo la kukosa choo kwa muda mrefu, (constipation) huweza kumpata mtu yeyote. Kuna watu wanaopata choo mara tatu kwa siku, wengine hupata mara chache kwa wiki. Kwa wale wanaofika siku tatu bila kupata choo huchukuliwa ni muda mrefu sana hivyo wako katika hatari.
Kuna baadhi ya mambo ambayo huchangia kukosa choo kwa muda mrefu/choo kigumu, na hivi ni baadhi ya vyanzo vinavyoweza kusababisha tatizo hilo;
*Msongo wa mawazo
*Ubovu wa lishe
Matumizi ya vyakula vilivyosindikwa sana, sukari, nafaka iliyokobolewa, pombe, huleta ugumu kwanye umeng'enywaji .
*Kutoshughulisha mwili (kutokufanya mazoez)
Utafiti unaonesha watu wanaotumia muda mwingi wakiwa wamekaa hasa ofisini wanaongoza kwa kupata matatizo ya kukosa choo kwa mda mrefu.
*Matumizi ya baadhi ya vidonge
*Matatizo ya tezi ya thyroid na matatizo mengine ya homoni:
Matatizo kama kisukari, kukoma hedhi, maumivu kabla ya hedhi.
*Upungufu wa magnesium
Madhara ya kukosa choo kwa mda mrefu
*Tumbo kuuma
*Tumbo kujaa gesi
*Bawasiri(kuota kinyama sehem ya haja kubwa
*vidonda kwenye utumbo mdogo na mpana
Fanya mambo haya yafuatayo ili kuzuia tatizo la kukosa choo kwa muda mrefu;
. Kula zaidi chakula chenye nyuzinyuzi kama maharage, mboga za majani,
matunda, nafaka nzima
. Kunywa maji mengi
. Fanya mazoezi ya mwili
. Jaribu kudhibiti msongo wa mawazo
. Usiahirishe kwenda chooni
. Jaribu kuweka ratiba maalumu ya kujisaidia, hasa baada ya kula.
Kama hautapata matokeo yoyote yale bas tutafute tukusaidie kwa haraka sana kupitia
Call:0744657095
WhatsApp: 0712043500
Tunapatikana dar es salaam kwa walioko mikoani tuwasiliane namna yakukusaidia
Read more